Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Okwi hawatanii waichakaza Coastal mabao 8-1

56367 Pic+matokeo

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WASHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wameisambaratisha Coastal Union baada ya wachezaji hao wawili kufunga magoli sita peke yao katika ushindi wa 8-1 katika mchezo huo.

Kagere na Okwi wameifunga magoli matatu kila mmoja huku Hassan Dilunga na Clatous Chama wakifunga moja moja.

Katika mchezo huo washambuliaji wa Simba waliweza kuipelekesha safu ya Ulinzi ya Costal Union kiasi cha kuwafanya mara kwa maa kushambulia.

Dakika 62 Coastal walifanya mabadiliko alitoka Ibrahim Ame na kuingia Bakari Mtwiku.

Wakati huo huo Simba walifanya mabadiliko dakika 67 kwa kumtoa Rashid Juma na kuingia Hassan Dilunga.

Dakika 69 Simba ilipata kona baada ya kipa wa Coastal, Soud Abdallah kucheza mpira wa Tshabalala.

Kona hiyo ilipigwa na Clatous Chama moja kwa moja kati na Meddie Kagere alipiga kichwa kichoenda moja kwa moja wavuni.

Coastal walionekana kupoteana na kuanza kuzozana mara kwa mara na muamuzi Jonesia Rukia.

Dakika 74 kagere aliifungia Simba goli la tano baada ya kupokea pasi mpenyezo kutoka kwa Hassan Dilunga.

Mabeki wa Coastal walizani Kagere ameotea katika goli hilo lakini muamuzi Jonesia Rukya aliweka kati.

Dakika 78 Simba walifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Said Ndemla na kuingia Mohammed Ibrahim.

Mabadiliko hayo yalionyesha kuwa na tija kwani dakika 80 Mohamed Ibrahim alipanda na mpira kwa spidi na kupiga pasi kwa nje na kukutana na Dilunga aliyepiga shuti moja kwa moja na kuifanya Simba kupata goli la sita.

Simba walizidi kushambalia zaidi katika lango la Coastal huku wapinzani wao wakionekana kuzidiwa kila idara.

Dakika 82 Simba walipata goli la saba kupitia kwa Meddie Kagere baada ya kuonganisha krosi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala'.

Dakika 90 Clatous Chama aliifungia Simba goli la nane na kuwafanya watoke na ushindi mnono uwanjani.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz