Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere: Kocha ndiye huamua nani atakayecheza

KAGERE Kagere: Kocha ndiye huamua nani atakayecheza

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

OKTOBA 4, ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa kinara wa mabao msimu uliopita Meddie Kagere kufunga bao kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma wakati timu yake ikishinda mabao 4-0, dhidi ya JKT Tanzania huku akifanikiwa kuweka kambani mabao mawili.

Tangu hapo Kagere amekuwa mchezaji wa kuanzia benchi na kusuasua kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na hata muda mwingine kukosekana kabisa.

Baada ya kukaa kwa zaidi ya miezi miwili na nusu bila kufunga bao Mnyarwanda huyo alikuja kufunga katika mechi ya juzi dhidi ya KMC akimtungua kipa, Juma Kaseja kwa mkwaju wa penalti bao moja ambalo liliwapa timu yake ushindi 1-0, ambao walikuwa wakihusaka kwa muda mrefu.

Katika kolamu yangu wiki hii ningependa kuzungumzia mambo mawili kwanza kukaa kwa siku nyingi bila kufunga mabao jambo ambalo tangu nimekuja kucheza soka hapa Tanzania ni nadra kuona linatokea kwa upande wangu na jambo la pili ni kuhusu nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kuhusu kufunga wanza ili ufanikiwe hilo lazima uwepo uwanjani lakini ukifuatilia mechi zetu nyingi ambazo nimeshindwa kufunga unaweza kukuta nyingi sipo lakini baadhi yake ambazo nipo nimetokea benchi na mara nyingine muda unabaki mchache kabla ya mchezo kumalizika.

Jambo la pili mara zote ninapokuwa uwanjani natamani kutimiza majukumu yangu ya kwanza ya kufunga lakini unaweza kukuta nafasi ambazo nakutana nazo nyingi si za wazi na muda wote nakuwa nalindwa na mabeki ndio maana naamua kutoa pasi kwa mchezaji mwenzangu aliyekuwa katika nafasi sahihi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz