Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Kibu waitakatisha Simba Kirumba

Kagereee Meddie Kagere akiifungia Simba goli la kwanza

Fri, 19 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabao mawili ya haraka haraka yaliyofungwa na Straika Meddie Kagere na moja la Kibu Denis yametosha kuwafurahisha mashabiki wa Simba SC, waliojazana katika uwanja wa CCM kirumba Jijini Mwanza, kushuhudia mchezo wa Simba dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting.

Simba ambayo kwa mara ya kwanza imecheza chini ya Kocha wake mpya Mhispania Pablo Franco Martin, wametandaza soka safi liliowaacha wapenzi wake wakitabasamu kila dakika ya mchezo.

Dakika ya 17 Meddie Kagere aliiandikia timu yake bao la kwanza akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Bernad Morrison ikiwa ni baada ya kosa kosa langoni mwa Ruvu Shooting.

Meddie Kagere alirudi tena nyavuni akiiandikia Simba bao la pili mnamo dakika ya 36 akimalizia mpira uliotemwa na Kipa Mohamed Makaka akiokoa shuti la Kibu Denis aliyepokea pasi safi kutoka kwa Bernad Morrison.

Simba iliandika bao la tatu katika dakika ya 44 likifungwa na Kibu Denis akitumia vyema faida iliyotengenezwa na Meddie Kagere aliyemhadaa kipa na kukwepa krosi ya chini chini iliyochongwa na Shomari Kapombe.

Dakika ya 4 Bernad Morrison aliangushwa katika eneo la hatari lakini mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara akapeta huku Uwanja ukilipuka kwa kelele kumlaumu refarii.

Tukio hilo lilisababisha Morrison kupewa kadi ya njano baada ya kumzonga mwamuzi na kumlazimisha kuwa alilofanyiwa lilikuwa ni kosa.

Morrison aliendelea kuonekana nyota wa mchezo akionyesha ufundi wake ambapo dakika ya 31 Cassian Ponera alionyeshwa kadi ya njano ya kumshika Morrison aliyekuwa akijaribu kumtoka.

Kipindi cha pili Simba waliingia kwa kuupoza mchezo pengine baada ya kuona tayari wanaongoza magoli matatu.

Dakika ya 71 Ruvu waliandika goli la kufutia machozi kupitia kwa Mkongwe maguli baada ya walinzi wa Simba kufanya uzembe wa kumkaba.

Dakika ya 72 Simba walipata penati baada ya Kibu Denis kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la 18 na Erasto Nyoni akashindwa kuweka mpira wavuni baada ya mlinda mlango wa Ruvu Mohamed Makaka kucheza penati hiyo.

Kwa ushindi huo Simba inabaki katika nafasi ya pili ikiwa na alama 14 baada ya michezo sita na kinara akiwa ni Yanga mwenye alama 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live