Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Dube watauana VPL

Dube Zoezi Data Kagere, Dube watauana VPL

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

UKIACHANA na vita ya kuwania ubingwa msimu huu pamoja na ile ya kutokushuka daraja kuna ushindani mwingine wa kuwania tuzo ya mfungaji bora.

Wachezaji wanaopewa nafasi kubwa katika ushindani huo ni washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao 11, John Bocco mwenye tisa na Prince Dube wa Azam anayeshika nafasi ya pili na mabao kumi.

Kutokana na kasi hiyo ya washambuliaji hao kutakuwa na mchuano mkubwa kwenye michezo 12, ambayo Simba wamebaki nayo wakati Azam wamebakiwa na mechi nane.

Katika mechi ambazo wamebakiwa nazo Simba, Kagere na Bocco rekodi zinaonyesha wamezifunga timu zote ambazo wanakwenda kukutana nazo.

Timu 12, ambazo Simba wanakwenda kukutana nazo ni, Mwadui, Kagera Sugar,

Gwambina, Dodoma Jiji, Yanga, Coastal Union, KMC na Polisi Tanzania.

Nyingine Mbeya City, Ruvu Shooting, Azam na Namungo.

Kama Kagere na Bocco wataendeleza moto wao huo wa kuzifunga timu hizo mmoja wapo naweza kutwaa tuzo ya mfungaji bora msimu huu. Wakati huo huo Dube na Azam yake wamebakiwa na michezo nane.

Mechi hizo ambazo wamebaki nazo watacheza dhidi ya Dodoma, Yanga, KMC, Biashara United, Gwambina, Namungo, Simba na Ruvu Shooting.

Dube ambaye alikosa mechi nyingi za mzunguko wa kwanza kutokana aliumia rekodi zinambana kwani katika mechi nane ambazo Azam wamebaki nazo hajaifunga hata timu mmoja.

Kutokana na makali yaliyoonyesha na Dube, yamemuibua Kagere amesema hana wasi wasi wowote katika mbio hizo kwani ana malengo amejiwekea.

Kagere alisema malengo yake ya kwanza ni kuisaidia timu kufikia malengo yake ya kutwaa ubingwa wa ligi na kufanya vizuri katika mashindano mengine.

Alisema baada ya kufanikisha hilo mafanikio mengine huwa yanakuja yenyewe ikiwemo hilo la kuibuka mfungaji bora wa ligi kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita.

“Baada ya hapo ndio nataka kufikia malengo yangu ya kufunga mabao ambayo nitafikia idadi ile ambayo nilimaliza nayo msimu uliopita na nikifanikiwa kufikia hapo ndio nitakuwa na malengo ya matamanio,” alisema na kuongezea;

“Sina wasi wasi wowote katika mbio hizi za ufungaji bora licha ya changamoto ya nafasi ya kucheza katika kikosi chetu na jinsi kilivyo naimani nitafikia malengo yangu.”

Kagere ndiye mfungaji bora wa misimu miwili iliyopita msimu wake wa kwanza 2018-19 alimaliza na mabao 23, msimu uliopita alimaliza na mabao 22.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz