Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagere, Dube wajiangalie

Meddie Kagere Scored For Simba Sc Vncm1722tkk41dxt5oibu2psh Kagere, Dube wajiangalie

Sun, 18 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By SADDAM SADICK UKIACHANA na wachezaji Meddie Kagere (Simba) na Prince Dube wa Azam FC, nyota wa Gwambina FC, Meshack Abraham naye ameonekana kuja kwa kasi katika Ligi Kuu kutokana na kuwatesa makipa.

Hadi sasa Dube anayekipiga Azam FC ndiye kinara wa mabao kutokana na kufunga mabao sita baada ya mechi sita, huku Kagere akifuatia kwa mabao manne mechi tano.

Hata hivyo Abraham ambaye ni msimu wake wa kwanza Ligi Kuu juzi akiisaidia timu yake ya Gwambina kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar aliweza kutupia bao lake la tatu msimu huu.

Mbali na idadi hiyo kwa kinda huyo, lakini pia aliweka rekodi ya kufunga katika mechi mbili mfululizo akianza dhidi ya Ihefu alipofunga mabao mawili ambayo yaliipa alama tatu timu yake.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Novatus Fulgence alisema licha ya kwamba nyota huyo hatajwi, lakini amekuwa moja ya wachezaji kikosini wenye faida katika mafanikio hadi sasa.

Alisema kutokana na kasi aliyoanza nayo huenda huko mbeleni akafanya makubwa zaidi kwani uwezo na ubunifu alionao uwanjani anaweza kushindana na maproo wa timu yoyote.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz