Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera ukizubaa unaachwa

Ihefu Wlcome Kagera Kagera ukizubaa unaachwa

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la ufundi la Kagera Sugar, limewachimba mkwara wachezaji wa timu hiyo likiwaambia kwamba yeyote atakayezubaa na kushindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi, basi ajue ataachwa katika dirisha dogo.

Kagera iliyotoka kupata sare ya 1-1 na KMC, kwa sasa ipo katika nafasi ya saba ikikusanya pointi 13 kutokana na michezo 10 na kocha wa timu hiyo, Mecky Mexime amesema wanafanya tathmini ya mwisho ya kikosi hicho kabla ya dirisha kufunguliwa Desemba 16 akipanga kufyeka wachezaji wasiopungua wanne, ili kupisha nyota wapya wa kuchukua nafasi zao kwa nafasi tatu tofauti.

Akizungumza nasi, Maxime alisema kwa sasa nguvu nyingi wamezielekeza kwenye mechi zinazofuata lakini wakati mechi hizo zikiendelea watakuwa wakifanya tathimini ya kikosi kwa ajili ya dirisha dogo, ili kuimarisha kikosi kwani kuna baadhi ya wachezaji wameshuka kiwango na hawajitumi.

“Dirisha dogo bado halijafunguliwa, kwa sasa tunazingatia michezo iliyo mbele. Kila mchezo unatupa picha na tathimini mpya kikosini,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live