Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera hesabu zipo robo ASFC

Kagera Sugar Players Kagera hesabu zipo robo ASFC

Mon, 1 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kukabiliwa na kibarua kigumu Ligi Kuu, benchi la ufundi la Kagera Sugar limesema hesabu zao kwa sasa ni kufuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Kagera inatarajiwa kuwa wageni wa Namungo katika mchezo wa 16 Bora wa michuano hiyo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Lindi kuanzia saa 2:00 usiku na kama itapata ushindi itafuzu kwenda robo fainali.

Kocha Msaidizi wa Kagera, Marwa Chambeli alisema wameanza maandalizi tangu Machi 19 na lengo ni kufanya vizuri ugenini mbele ya Namungo ambao ni mchezo mgumu na wakimaliza kibarua hicho wanaamishia nguvu kwenye mechi za Ligi Kuu.

“Tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku tano na tayari wapo kambini Bukoba tunaendelea na matizi tunajiweka fiti kwa mchezo wa ASFC dhidi ya Namungo ugenini na kujiandaa kwa michezo ya ligi,” alisema Chambeli, huku kiungo wa timu hiyo, Geofrey Manyasi, alisema benchi la ufundi chini ya Fredy Felix ‘Minziro’ limewataka wachezaji kila mchezo wafanye vizuri wakianza na Namungo.

"Tunahitaji kutinga robo fainali na kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara, bahati nzuri timu ipo pazuri na imejengwa na upendo, umoja na ushirikiano hivyo morali ipo juu na kila mchezaji anajituma mazoezini kuonyesha yupo tayari kujipambania na kuipambania timu.”

Chanzo: Mwanaspoti