Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera Sugar yaendeleza ubabe kwa Tz Prisons

Kgera X Prisons Kagera Sugar yaendeleza ubabe kwa Tz Prisons

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rekodi ya Kagera Sugar kuifunga Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine Mbeya imeendelea baada ya leo kuibomoa bao 1-0 na kumaliza kibabe dakika 90.

Kagera Sugar inaondoka jijini Mbeya na jumla ya pointi nne baada ya awali kutoshana nguvu ya mabao 2-2 dhidi ya Mbeya City na leo inatakata kwa ushindi huo.

Bao pekee la Straika Meshack Abraham dakika ya 86 ndilo la kwanza kwake msimu huu ambalo limeisaidia Kagera Sugar kuvuna alama tatu muhimu.

Katika mchezo huo kadi mbili za njano zilitolewa kwa wachezaji Oscar Paul na Samson Mbangula katika dakika ya 17 na 66.

Kipigo cha bao 1-0 walichopata Tanzania Prisons dhidi ya Kagera Sugar leo kinafikisha mechi nane kati ya michezo 15 walizokutana dhidi ya wapinzani hao katika uwanja wa Sokoine Mbeya, huku matokeo mazuri kwao ikiwa ni sare.

 Katika mechi hizo zote Prisons haijawahi kuwafunga Kagera Sugar inapokuwa nyumbani huku ikishinda miwili katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Katika michezo 15 ukiwamo wa leo Jumatatu Novemba 21 walizokutana timu hizo, Kagera Sugar imeshinda mitano, sare nane na kupoteza miwili

Pia huo unakuwa mchezo wa tano mfululizo kwa Maafande hao wa jijini hapa bila kupata pointi tatu tangu waliposhinda kwa Polisi Tanzania Oktoba 25 mabao 2-1, ikiwa ni sare mbili dhidi ya Ruvu Shooting na Namungo na vipigo vitatu kwa Coastal Union 2-0, Geita Gold 4-2 na leo 1-0.

Matokeo hayo yanaiporomosha Prisons hadi nafasi ya 12 kwa alama 14 katika msitali wa njano, huku Kagera Sugar wakichumpa nafasi ya tisa kwa alama 15.

Prisons pia inaweka rekodi ya kufungwa kila mechi katika michezo yake tano mfululizo akiruhusu saba tangu mechi yake na Ruvu Shooting iliyomalizika kwa sare ya 1-1.

Katika hali isiyo ya sintofahamu leo jukwaa la Tanzania Prisons lilifurika nyuki na kusababisha mashabiki wa timu hiyo kuhamia eneo lingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live