Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera Sugar waitembezea kichapo Prisons Uwanja wa Kaitaba

IMG 6211.jpeg Kagera Sugar waitembezea kichapo Prisons Uwanja wa Kaitaba

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na Obrey Chirwa kwa penalti dakika ya 20 na Cleophace Mkandala dakika ya 68, wakati bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Khamis Mcha 'Vialli' dakika ya 72.

Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya saba, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake saba nafasi ya 14 katika ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: