Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera Sugar kumtema Makame

Makame Yanga Def Abdulaziz Makame ‘Bui’

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Kagera Sugar iko mbioni kuachana na kiungo wake, Abdulaziz Makame ‘Bui’ ikiwa ni miezi sita tangu aanze kukitumikia kikosi hicho akitokea Namungo aliyoachana nayo Julai mwaka jana.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo ililiambia Mwanaspoti kwamba, Makame amesitishiwa mshahara wa kila mwezi kutokana na kutohudhuria kambini tangu alipoondoka mwaka jana na kwenda Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Ally Masoud alisema “Kwa sasa siwezi kueleza sana juu ya hilo kwa sababu tumeelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu wa leo (jana) na KMC hivyo tutaongea baadae.”

Kwa upande wa Makame alisema ni kweli amepata barua ya kuhitajika kuhudhuria kwenye kituo chake cha kazi ingawa ataenda pindi tu atakapopata ahueni kwani bado anauguza majeraha yake ya goti.

Mwanaspoti linatambua Makame yupo kwenye mazungumzo ya kuachana na timu hiyo kwa kile kinachoelezwa kutofautiana na baadhi ya vigogo wa benchi la ufundi.

Chanzo: Mwanaspoti