Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera Sugar, Simba nani kutibua rekodi?

Simba Leo Bukoba Kagera Sugar waapa kutibua rekodi ya Simba

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rekodi ya kila timu kutopoteza mechi mfululizo za ligi hapana shaka inaongeza msisimko wa mechi baina ya Kagera Sugar na Simba leo kuanzia saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Kaitaba.

Timu hizo mbili zimeonyesha uimara wa kucheza mechi nyingi mfululizo za ligi katika siku za hivi karibuni bila kupoteza jambo linalofanya matokeo ya leo kusubiriwa kwa hamu na wengi kuona kama yatavuruga rekodi hiyo kwa timu mojawapo au itazidi kuboreshwa.

Wenyeji Kagera Sugar wanaingia katika mechi ya leo wakiwa wamecheza mechi tano mfululizo zilizopita za ligi bila kupoteza wakipata ushindi michezo mitatu na kutoka sare miwili huku Simba wakiwa wamecheza mechi tisa mfululizo bila kupoteza wakipata ushindi mara saba na sare mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live