Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera, Mtibwa washikilia ubingwa wa Yanga

Gamondi Yanga Ms Kagera, Mtibwa washikilia ubingwa wa Yanga

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu za Kagera Sugar, Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji ndiyo zimeushikilia ubingwa wa Yanga SC. Yanga SC inahitaji pointi 8 ili iweze kuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara tatu mfululizo.

Yanga SC imebakisha michezo mitano kumalizika kwa ligi hiyo. Katika michezo hiyo mitano, Yanga SC wanatakiwa kushinda michezo mitatu ili waweze kuwa mabingwa wa ligi hiyo.

Michezo hiyo ni dhidi ya timu za Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Dodoma Jiji. Yanga akipata matokeo ya ushindi katika michezo hiyo watafikisha pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Michezo miwili ya mwisho ni Tabora United na Tanzania Prisons. Michezo hii huenda ikawa ya kukamilisha ratiba kama watashinda michezo hiyo mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live