Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera, KMC hakuna mbabe Kaitaba

IMG 7628.jpeg Kagera, KMC hakuna mbabe Kaitaba

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Jana Novemba 22 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar walitangulia na bao la beki wake Mganda, Deus Bukenya dakika ya 49, kabla ya mshambuliaji Waziri Junior Shentembo kuisawazishia KMC dakika ya 74.

Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 16 na kupanda nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar sasa ina jumla ya pointi 13 na inasogea nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live