Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagera, JKT Tz hakuna mbabe Kaitaba

IMG 9045.jpeg Kagera, JKT Tz hakuna mbabe Kaitaba

Sun, 3 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jana Jumamosi Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

JKT Tanzania walitangulia na bao la Edward Songo dakika ya 22, kabla ya Mubarak Hamza kuisawazishia Kagera Sugar kwa penalti dakika ya 41.

Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya saba na JKT Tanzania inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 18 ingawa inabaki nafasi ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live