Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kagame Cup darasa kwa Yanga

KAGAME YANGA Mchezaji wa Yanga akizongwa na wachezaji nwa Atlabara FC

Thu, 5 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) jana Agosti 4,walishuka dimbani na kusuluhu katika mchezo wao wa Pili dhidi ya Atlabara FC ya Sudan Kusini,mchezo uliochezwa majira vya saa 1:00 Usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa,Dar es Salaam.

Licha ya kuwa Mashabiki wa Yanga wanaoneshwa kutofurahishwa na kiwango wala matokeo yanayotokea uwanjani kwa upande wa timu yao lakini Ziko Faida viongozi wa Yanga wanazipata kwenye michuano hii,hali kadhalika mashabiki wanatakiwa pia walijue hili.

Mosi, Wanajua Ubora wa vijana wao.Wanajua Pengo lililopo kati ya wachezaji wanaoanza na wale wa akiba.Sote tunafahamu kuwa Timu ya Yanga imepeleka Kikosi cha wachezaji ambao hawapati nafasi mara kwa mara na wale wa timu za vijana katika kushiriki Mashindano haya.Tofauti na Watani wao ambao wao hawashiriki kabisa Mashindano haya,Klabu ya Simba.

Kwa msingi huo wanapata kujua ubora wa hawa vijana pindi inapokuja katika levo ya ushindani kwa maana ya uwezo na utayari wao wa kupandishwa timu ya ligi kuu ili yanga waweze kufaidika na matunda ya uwekezaji wao katika timu hii ya vijana.

Lakini pia kujua Pengo lililopo kati ama baina ya wachezaji wanaoanza kikosi cha kwanza na wale waliopo katika benchi. ni kupitia mashindano haya tu ndipo ambapo wanaweza kufahamu tofauti hizo kwa kuwa wao ndio wakati wanaopata nafasi na kumshawishi mwalimu ni kwa nini wanastahili kuendelea kubaki na kupewa nafasi.

Pili,Wanajua pia Ubora wa makocha wa Timu zao za vijana.Kutokana na kiwango kinachooneshwa na vijana hawa wakati huu mashindano yakiendelea ambayo yanatoa nafasi kwao kuonyesha vipaji vyao kwa kuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambapo wanaopata nafasi mara kwa mara hawajajumuishwa katika kikosi cha mashindano haya.Viongozi kupitia Mashindano haya wanaona ubora wa vijana wao na kutathmini uwezo wa walimu wa timu za vijana,hivyo kupata nafasi ya kufanya maamuzi.

Vile vile wanaona Mahaba mazito ya Mashabiki wao wanaoendelea kulipa Viingilio vyao kwenda kuishangilia Timu yao hata kama inacheza vibaya na kushindwa kupata matokeo.

Wakati bado tupo na tunaendelea na Mashindano hili linapaswa lisisahaulike na tuitumie hii michuano kama darasa kuboresha na kupata kilicho bora kwa kuwa tofauti na mashindano haya sioni ni wakati mwingine upi Yanga wangepata nafasi kama hii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live