Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaduguda: Mangungu hana weledi na mpira

Murtaza Mangungu Kaduguda: Mangungu hana weledi na mpira

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi Simba, Mwina Seif Kaduguda 'Simba wa Yuda' amesema kuwa tatizo kubwa lililopo Simba Sc ni katiba yao kwani inaruhusu mtu yoyote kuwa kiongozi wa klabu hata kama hana weledi na uzoefu wa masuala ya soka.

Kaduguda amesema Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Ally Mangungu hana uzoefu na masuala ya soka na ndicho kitu kinachoifanya Simba kushindwa kufanya vizuri.

“Nimemuona ni mtu mwenye busara, amechelewa, hakutakiwa hata kuiongoza Simba kwa miaka saba, hakustahili. Kwa miaka saba aliyokaa Simba alitakiwa awavute watu wenye ueledi na mpira sio Mangungu. Mangungu amekuwa mbunge wa Kilwa Kaskazini, hajawahi kushughulika na mpira unamleta kuja kushughulikia masuala ya soka Simba?

“Yeye anajua mambo ya utawala na utawala wa mpira sio utawala wa kwenda sokoni au bunge. Ni shida lakini kama tunataka kutibu soka letu lazima tuwe wakweli. Haiwezekani Simba ina umri wa miaka 88 haijawahi kuwa Bingwa wa Afrika, tunakaa tu maneno maneno, mtu akisema ukweli anaonekana ana matatizo?

“Tatizo la Simba bali ni wanachama, ni mambumbumbu hawataki kujielimisha, haiwezekani wewe shabiki unasema una asilimia 51 za hisa halafu maamuzi umemwachia mtu mwenye asilimia 49.

“Katiba inataka kiongozi ilimradi awe na kadi tu ya uanachama wa klabu, inawezekanaje kiongozi hajui mpira akaongoza mpira? Kama huwataki wanachama wenye ueledi na mpira na wewe huwa ueledi wa mpira, huwezi kufika kokote, ndiyo haya yanatokea.

“Mtu hajawahi kushughulikia mpira hata level ya kata, tarafa, wilaya wala mkoa halafu leo anakuja kwenye dude kubwa kama Simba au Yanga kwa sababu tu ana kadi ya chama, hapo kuna shida.

“Mangungu hajawahi kuongoza mpira kokote, kaja kujifunzia Simba. Simba ni kama chuo kikuu, huwezi kuingia wakati hujawahi kufika hata kidato cha nne,” amesema Kaduguda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: