Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadi zamponza Erik Ten Hag

Ten Hag Card Kadi zamponza Erik Ten Hag

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amepigwa marufuku kusimama pembeni ya mstari wa uwanja kwenye mechi ya inayofuata ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton baada ya mapumziko ya kimataifa badala yake atakuwa jukwaani.

Ten Hag amepewa adhabu hiyo baada ya kufikisha kadi tatu za njao kutokana na mabadiliko ya sheria za Ligi Kuu England msimu huu.

Mdachi huyo alilimwa kadi ya njano kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Luton City baada ya kupishana kauli na marefa nje ya uwanja dakika za lala salama katika Uwanja wa Old Trafford.

Ten Hag alikutwa na maswahibu hayo baada ya kutokubaliana jambo na waamuzi wa mchezo akiwemo Graham Scott, inamaanisha kwamba Mdachi huyo atafungiwa mechi moja ya ligi ambayo itachezwa ugenini dhidi ya Everton Novemba 26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live