Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kadi moja tu hawachezi Boxing Day

Kadi Moja Tu Kadi moja tu hawachezi Boxing Day

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Zaidi ya wachezaji 30 wapo hatarini kukosa mechi za Ligi Kuu England zitakazochezwa Boxing Day baada ya kufikisha kadi nne za njano.

Raundi ya mwisho za mechi zitachezwa kabla ya Sikukuu ya Krismasi kuanzia Alhamisi na Jumapili na jumla ya timu 18 zitakuwa uwanjani zikimenyana.

Mechi kati Manchester City na Brentford imehairishisha kutokana na Manchester City kushikiri mashindano ya Kombe la Dubia kwa ngazi ya klabu.

Wachezaji wa Ligi Kuu watapewa adhabu ya kukosa mechi moja endapo watafikisha kadi tano za njano kabla ya kufikisha mechi 20, huku wachezaji 36 mpaka sasa tayari wana kadi nne za njano, hivyo wanatakiwa kuwa makini. Pia, wale wachezaji ambao watafikisha kadi 10 za njano kabla ya mechi 33 watakosa mechi mbili.

Kati ya hao wachezaji 36, 31 tu ndo wanastahili kucheza mechi ya 18 ya Ligi Kuu. Wawili kati ya wale ambao hawatacheza katika raundi ya pili ya ratiba ya mechi ya ligi ni wachezaji wa Brentford, Kristoffer Ajer na Saman Ghoddos.

Nahodha wa Luton, Tom Lockyer ana kadi nne za njano mpaka sasa msimu huu, hata hivyo, bado anaendelea na matibabu baada ya kupata mshtuko wa moyo uwanjani, wakati wa mechi yao dhidi ya Bournemouth Jumamosi iliyopita. Mechi hiyo ilisimamishwa na itachezwa tena hapo baadaye.

Beki wa Crystal Palace, Joel Ward na kiungo wa Newcastle Joelinton pia wana kadi nne za njano, hata hivyo, wemepata ahueni kwa sababu wapo nje ya dimba kutokana na majeraha ya misuli ya paja na hawatarajiwi kurejea mapema. Kwa mujibu wa ripoti Haijafahamika watakaa nje ya dimba kwa muda gani.

Wachezaji wengine wa Crystal Palace, Joachim Andersen na Jordan Ayew ni miongoni waliokuwa na kadi nne za njano, huku wachezaji wa Brighton, Lewis Dunk, Billy Gilmour na Kaoru Mitoma nao wana kadi nne za jano.

Aidha kwa upande wa Ayew, awali alikuwa na kadi sita za njano, lakini tayari ametumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi moja, na alikosa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester City na kuambulia sare ya mabao 2-2. Ligi Kuu imethibitisha kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Ghana ana rekodi ya kuwa na kadi nne za njano na moja nyekundu.

Aston Villa ina matumaini wachezaji wake, Matty Cash Jhon Duran na John McGinn wataepuka janga hilo, hivyo wanatakiwa kucheza kwa nidhamu, hadi tunaenda mitamboni ilitarajia kucheza dhidi ya Sheffield United jana.

Brentford ndio yenye wachezaji wengi zaidi wenye kadi nne za njano, Anel Ahmedhodzic, Jayden Bogle, Gustavo Hamer, William Osula hivyo wapo katika hatari ya kufungiwa mechi.

Mchezaji wa West Ham, Vladimir Coufal, atakuwa makini zaidi watakapocheza dhidi ya Manchester United, ili asilimwe kadi kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu.

Naye mchezaji wa Fulham, Antonee Robinson ataomba asikumbane na kadi katika mechi dhidi ya Burnley. Mechi hizo za Ligi Kuu England zitachezwa leo viwanja tofauti.

Fowadi wa Arsenal, Kai Havert, Marco Senesi anayekipiga Bournemouth, Ashley Young na Abdoulaye Doucoure wote kutoka Everton, Darwin Nunez (Liverpool), Issa Kabore (Luton City) Jamaal Lascelles na Sean Longstaff kutoka Newcastle, Orel Mangala na Ibrahim Sangare wa Nottingham Forest, mastaa wa Tottenham, Cristian Romero na Pape Matar Sarr, wote wana kadi nne za njano.

Kuna mechi moja tu itakayochezwa katika mkesha wa Krismasi, mchezo huo utakuwa kati ya Wolves na Chelsea. Baadhi ya Wachezaji wa Wolves, Rayan Ait-Nouri na Hwang Hee-Chan, pamoja na mastaa watatu wa The Blues Enzo Fernandez, Cole Palmer, Raheem Sterling wote wana kadi nne za njano.

Chanzo: Mwanaspoti