Baada ya Simba kushinda bao 1-0 dhidi ya Vipers FC jumamosi iliyopita na kuchukua alama tatu katika mchezo wa hatua ya Mkaundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa Kuna Kiongozi Mmoja wa Benchi la Ufundi la Simba ambae jina lake mpaka wakati huu halijatajwa, alibaki Uganda kwa ajili ya kuwasoma wapinzani wao Vipers kabla ya kurudiana nao Machi 7 Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo inatanabaisha kuwa hatua hiyo imekuja ikiwa ni ushauri wa Robertinho ambaye alidai anawajua kuwa Vipers hubadilika badilika Mechi na mechi hivyo ni vema akawa anajua wanafanya nini.
Simba SC wako kundi C Sambamba na Raja Casablanca ambae ndio kinara anaeongoza kundi akiwa na alama 9, Horoya wenye alama 4, Simba SC wana alama 3 huku Vipers wakiburuza mkia na alama 1.