Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kabwili Yupo Zake Tabata FC

Kabwili Kabwili Yupo Zake Tabata FC

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kutoonekana ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, golikipa Ramadhan Kabwili, ameonekana akicheza fainali ya Kombe la Ng’ombe akiwa na Tabata FC.

Kabwili ambaye aliondoka kambini tangu Yanga ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa Novemba 20, 2021, mpaka leo hajaonekana akiwa na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Juzi Jumapili, Spoti Xtra lilimshuhudia kipa huyo akiwa kwenye kikosi cha Tabata FC ambacho kilicheza mchezo wa fainali ya kombe la Ng’ombe dhidi ya Tabata Future kwenye Uwanja wa Tabata Shule uliopo Tabata jiji Dar.

Mchezo huo ulimalizika kwa Tabata FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuchukua zawadi ya ng’ombe huku Tabata Future wakiambulia mbuzi wawili ambao ni zawadi ya mshindi wa pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live