Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KVZ ina ukuta wa chuma Ligi Kuu Zanzibar

KVZ Zanzibar KVZ ina ukuta wa chuma Ligi Kuu Zanzibar

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Safu ya ulinzi ya KVZ ndiyo mpaka sasa haijaruhusu bao kwenye Ligi Kuu Zanzibar ikiwa imeshacheza michezo minne.

Ukuta wa timu hiyo unaoongozwa na mlinda mlango Ajrif Ali akisaidiwa wa walinzi Salum Khamis Gado, Abrahma Saidi (Mani), Ali Saleh Machupa na Simai Mcha "Pepe" wanaifanya KVZ kuwa timu pekee ambayo haijaruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye ligi hiyo hadi sasa.

wakiwa wamecheza dakika 360, wameisaidia timu yao kupata pointi 10 kwenye michezo minne, alama sita wakizipata Kisiwani Pemba katika Uwanja wa FFU Finya waliposhinda dhidi ya Maendeleo na Chipukizi.

FFU Finya ni uwanja ambao unatoa wakati mgumu kwa timu kutoka Unguja kuondoka na alama zote kwa michezo ambayo timu kutoka huku zimecheza.

Licha ya kuwa na safu bora ya ulinzi ambayo haijaruhusu bao lakini KVZ imekuwa butu katika eneo la ushambuliaji kwani katika michezo yote minne wamefunga mabao manne wastani wa bao moja kwa kila mchezo.

KVZ inatajwa kuwa miongoni mwa timu ambazo zinawania ubingwa msimu huu kutokana na muendelezo wake kuanzia msimu uliomalizika na ubora wa timu waliyonayo.

Msimu uliopita, KVZ ilimaliza nafasi ya pili kwa alama 65, ikipoteza mechi mbili nyuma ya KMKM iliyotwaa ubingwa kwa alama 69.

Kwa sasa KVZ ikiwa inanolewa na kocha Ali Mohammed Ameir inashika nafasi ya pili kwa pointi 10, sambamba na vinara JKU SC yenye pointi 10 pia.

Chanzo: Mwanaspoti