Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMKM yapigwa tena, yatema ubingwa ZPL

Fxfxfxfcx KMKM yapigwa tena, yatema ubingwa ZPL

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Maafande wa KMKM, imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika mechi za lala za Ligi Kuu Zanziba (ZPL) na kuutema rasmi ubingwa baada ya jioni ya jana kufungwa mabao 2-1 na KVZ.

Watetezi waliokuwa wanalishikilia taji kwa msimu wa tatu mfululizo, walikumbana na kipigo hicho kwenye Uwanja wa Mao A, mjini Unguja ikiwa ni wiki moja tu, tangu walipolala mbele ya Mafunzo kwa idadi kama hiyo.

Kipigo hicho kimeiacha timu hiyo kusalia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 na michezo miwili mkononi, ambayo hata ikishinda yote haiwezi kufikia pointi ilizonazo JKU inayoongoza msimamo kwa muda mrefu na alama 62.

Dalili mbaya kwa KMKM zilianza kuonekana mapema kwa bao la dakika ya kwanza tu ya mchezo huo, lililowekwa kimiani na Sabri Dahari Omari kabla ya Suleiman Mwalim Abdallah kuongeza la piki dakika ya 35 likiwa ni la 20 kwa nyota huyo kwa msimu huu.

Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko kabla ya kipindi cha pili kilianza kwa KMKM kucharuka kusaka mabao ya kusawazisha

na jitihada hizo zilizaa matunda dakika ya 78 kwa Firdaus Seif Amour alipofunga bao la kufutia machozi kwa timu hiyo.

Ushindi huo umeifanya KVZ kufikisha pointi 53 baada ya mechi 28 ikiwa nafasi ya nne nyuma ya KMKM.

Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa FFU Finya, kisiwani Pemba Zimamoto ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Chipukizi na kufikisha pointi 59 ikiifukuzia JKU kileleni.

Mabao ya Mgaza Seleman Ramadhan dakika ya 14 na la Suleiman Said Juma dakika ya 84 yalitosha kuizamisha Chipukizi iliyosaliwa na pointi 39 baada ya mechi 28 ikiganda nafasi ya sita.

Ligi hiyo iliyobakiza mechi za raundi mbili kabla ya msimu kukamilika itaendelea tena kesho jioni.

Chanzo: Mwanaspoti