Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMKM watupwa nje Ligi ya Mabingwa Afrika

KMKM CAF.jpeg KMKM watupwa nje Ligi ya Mabingwa Afrika

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya KMKM ya Zanzibar imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-1 na wenyeji, St George katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali usiku wa Jumapili Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mabao ya St George yamefungwa na viungo Dawit Tefera Alemu dakika ya 49, Natnael Zeleke Tadesse dakika ya 65 na mshambuliaji Abel Yalew Tilahun dakika ya 79, baada ya KMKM kutangulia na bao la mshambuliaji wake, Salum Akida Shukuru dakika ya 24.

Kwa matokeo hayo, St George wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2 kufuatia kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam na sasa watamenyana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live