Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMKM, JKU hapatoshi mechi Ngao ya Jamii

KMKM CAF.jpeg Kikosi cha KMKM

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Joto la fainali ya Ngao ya Jamii kati Maafande wa KMKM dhidi ya JKU ikipanda, Makocha wa pande zote mbili wametambiana ambapo kila mmoja ameahidi kumuheshimu mpinzani wake na kushinda mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu na Mashabiki wa Soka Visiwani Zanzibar.

Mchezo wa Ngao ya jamii kati ya KMKM na JKU unatarajiwa kuchezwa kesho katika uwanja wa Mao Tsung majira ya saa kumi jioni huku Mgeni rasmi katika mchezo huo akitarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar.

Wakizungumza na katika Mkutano na Waandishi wa Habari Kocha Mkuu wa Timu ya JKU Salim Ali Haji pamoja na Meneja Mkuu wa timu ya KMKM Khamis Haji Khamis wamesema kuwa mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vyao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live