Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC yazizidi ujanja Simba, Yanga kwa kipa huyu

Kipa 18198 KMC yazizidi ujanja Simba, Yanga kwa kipa huyu

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa KMC FC, upo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Kipa wa timu ya Taifa ya Burundi, Fabien Mutombora kwa msimu ujao.

Mutombora aliyekuwa kipa namba moja wa klabu ya Vipers ya Uganda amemaliza mkataba wake na sasa ni mchezaji huru na muda wowote KMC itamtangaza kwenda kuchukuwa nafasi ya makipa walikuwepo msimu uliopita Denis Richard na Wilbol Maseke.

Taarifa zilizoifikia kutoka ndani ya timu hiyo ni kuwa, viongozi wanachukuwa hatua ya kutafuta makipa wawili akiwemo mmoja kutoka nje ambaye ni Mutombora na mzawa ambaye bado wako katika kuangalia.

Mtoa habari huyo amesema wanahitaji kuachana na makipa wote wa msimu uliopita kwa kuhakikisha wanaimarisha nafasi hiyo kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Abdulhamid Moalin

“Jambo muhimu kocha amekuwa akisisitiza juu ya usajili ni kuangalia zaidi nafasi ya kipa, tayari tunaendelea na mazungumzo na kipa huyo kutoka Burundi, tuko katika hatua nzuri na ikifika muda wake tutaliweka wazi,” amesema Chanzo hicho.

Hivi karibuni Spotileo lilifanya mahojiano ya Mtendaji Mkuu wa KMC FC, Daniel Mwakasungula aliweka wazi kuwa wanahitaji kufanya maboresho katika nafasi ya kipa baada ya kuangalia tathimini ya timu yao.

“Tulipokea ripoti kutoka kwa kocha wetu, akituhimiza kufanya maboresho ya kipa hilo tupo kwenye mchakato kuhakikisha tunaweza kupata mtu sahihi akatusaidia kwa msimu mpya,” alisema Mwakasungula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live