Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC yawachimba mkwara Tabora United

Kmc Yapiga KMC yawachimba mkwara Tabora United

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya KMC FC, imetuma salamu kwa Tabora United ambayo watacheza nayo Oktoba 22, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

KMC ambayo juzi ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Nyumbu na kushinda 10-1, imesema hizo ni salamu kuelekea kuivaa Tabora United.

Ofisa Habari wa KMC, Khalid Chukuchuku, amesema: “Tunaendelea na mazoezi kwa ajli ya mchezo wetu ujao ambapo tutakuwa ni wagen dhidi ya Tabora United.”

“ Tunawaambia mapinzani watu wajipange maana tuko vizuri, tumetoka kucheza mechi ya kirafiki na Nyumbu na tumewaliza mabao 10-1, hii ni salamu tosha kwa wapinzani wetu kuwa wajipange.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: