Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC yajilipua kwa Geita Gold

KMC Geita KMC FC

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha KMC kinashuka uwanjani muda mfupi ujao kuvaana na Geita Gold huku kikiingia bila wakali wao wa mabao, Matheo Antony na George Makang'a.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Nyankumbu mkoani Geita kuanzia saa 10 jioni, ambapo Makang'a anaanzia benchi huku Matheo akikosekana kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika mchezo huo KMC inasaka walau ushindi wa kurejea nao jijini Dar es Salaam kutoka Kanda ya Ziwa baada ya kuchapwa bao 1-0 na Kagera Sugar mwishoni mwa wiki iliyopita.

KMC imepoteza michezo miwili mfululizo ikifungwa 1-0 na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na 1-0 mbele ya Kagera Sugar.

Leo Kocha wa KMC, Hitimana Thierry amemrejesha langoni kipa David Kissu baada ya Nurdin Barola kuruhusu bao kwenye mchezo uliopita, bao ambalo Hitimana alimtupia lawama kuwa ni uzembe binafsi.

Kikosi cha KMC: Kipa ni David Kissu, mabeki wa pembeni ni Kelvin Kijili na Hance Masoud, mabeki wa kati ni Sadala Lipangile na Andrew Vincent huku viungo wakiwa ni Baraka Majogoro, Abdallah Masoud na Emmanuel Mvuyekule, mawinga ni Darueshi Saliboko na Nzigamasabo Steven huku mshambuliaji akiwa Waziri Junior.

Kikosi cha akiba ni Nurdin Barola, Boniphace Maganga, George Makang'a, Kenny Ally, Mohamed Samatta, Abdul Hillary, Cliff Buyoya, Ibrahim Ame na Isaac.

Chanzo: Mwanaspoti