Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC yaitahadharisha Namungo Ligi Kuu

D35691e8ec7465e1cc0a515817dd434c.png KMC yaitahadharisha Namungo Ligi Kuu

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa KMC, John Simkoko ametamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kesho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Simkoko alisema maandalizi makubwa waliyofanya ikiwamo kupata michezo ya kirafiki ni kati ya sababu za wachezaji wake kuwa na morali ya kuibuka na pointi tatu katika mchezo huo.

“Mchezo utakuwa na ushindani lakini kwakuwa tutakuwa nyumbani mipango yetu ni kuibuka na ushindi, tumefanya maandalizi ya kucheza mechi za kirafiki ambazo zimesaidia kuwajenga wachezaji wangu kwenye utimamu wa mwili,” alisema.

Simkoko alisema walicheza michezo kadhaa ya kirafiki ikiwamo dhidi ya Azam FC iliyokuwa na ushindani na kubaini udhaifu ambao ameshaufanyia kazi kwenye mazoezi.

KMC inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza michezo 17, ikishinda mechi sita, sare nne na kupoteza mechi saba. Inakutana na Namungo inayoshika nafasi ya 15 iliyocheza michezo 14 ikiwa na pointi 18, ikishinda michezo minne, sare sita na kupoteza michezo minne.

Chanzo: habarileo.co.tz