Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC yaichapa Mwadui

Kmc Pc Data KMC yaichapa Mwadui

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this Author KLABU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.KMC ndio walikuwa wa kwanza kupata mabao hayo kupitia kwa Emmanuel Mvuyekure kwa mkwaju wa penalti kisha Charles Ilanfya alikata mzizi zaidi na kufanya timu hiyo kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza.Katika kipindi cha pili Mwadui walionekana kubadilika na kuhitaji kupata mabao ya kusawazisha.Mabadiliko ya kuingia mshambuliaji mkongwe, yalionekana kusaidia kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira.Dakika 70 Mwadui walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Denis Richard na bao hilo liliwarejesha mchezoni Mwadui.Mabeki wa KMC, Andrew Vicent 'Dante', Lusajo Mwaikenda walikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha wanawazuia washambuliaji wa Mwadui katika dakika za mwisho.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz