Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC wanazitaka pointi 3 za Yanga

KMC VS YANGA AFRIKA Kikosi cha KMC

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wao leo jumatano dhidi ya Yanga, Kocha Msaidizi wa KMC, Ahmed Ally amesema kuwa mipango yao ni kupata pointi tatu au ikishindikana waipate moja.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Yanga tayari wakiwa wamekusanya pointi 14 na KMC wakiwa nazo 13.

Akizungumzia maandalizi yao, Ahmed amesema wamejiandaa kuelekea kwenye mchezo huo ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

“Timu ipo vizuri kuelekea kwenye mchezo wa leo na mipango yetu ni kuhakikisha tunavuna pointi tatu au ikishindikana tupate pointi moja.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu wana kikosi kizuri tumewaona kwenye mechi iliyopita hivyo tumeenda mazoezini na kuandaa mipango mipya kwa ajili ya mchezo huo.

“Makosa ambayo yalifanyika kwenye michezo iliyopita tumeyafanyia kazi na kuyamaliza hivyo hayawezi kujitokeza tena na mashabiki wetu tunawaahidi ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live