Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC waitangazia vita Coastal Union ufunguzi pazia la Ligi Kuu

KMC Vs Coastal Kikosi cha KMC FC wakiendelea kujifua kuelekea msimu mpya

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya KMC wamewapiga mkwara Coastal Union kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa kwanza msimu mpya utakaowakutanisha, kwani wana kikosi bora katika kukamilisha malengo yao.

KMC inatarajia kuwakabili Coastal Union Agosti 17 mwaka huu, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa ligi(mchezo huo ndio utakaofungua ligi kwa timu zote mbili).

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa: “Tunafahamu msimu ujao utakuwa na ushindani mkubwa kwani kila timu imejiandaa kiushindani, lakini siku zote KMC imekuwa ikihakikisha inafanya vizuri kwenye michezo yake.

“Malengo yetu makubwa ni kumaliza katika nafasi nne za juu jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu.

“Ukiangalia msimu huu tuna idadi kubwa ya maingizo mapya ya wachezaji ambao wote wana uzoefu wa kucheza ligi ya Tanzania na nje ya nchi, hivyo katika kujenga muunganiko wa wachezaji jambo hilo linakwenda vizuri.

“Niwatoe hofu mashabiki kuwa tuna timu nzuri na bora yenye ushindani kuelekea kuanza kwa msimu mpya.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live