Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC waipeleka Yanga Songea

KMC FC Kikosi cha KMC

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KMC ni kama wameangalia zaidi fursa ya kibiashara baada ya kuchagua kuupeleka mchezo wao dhidi ya Yanga kuchezwa Songea, eneo ambalo kwa muda mrefu hawajashuhudia michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara.

Katibu Mkuu wa klabu ya Kinondoni Municipal Council ‘KMC’ ya Dar es Salaam, Walter Harrison ameelezea sababu ya kwanini mchezo wao dhidi ya Yanga wa Ligi Kuu Bara utachezwa kwenye uwanja wa Maji Maji, Songea Mkoani Ruvuma.

Katibu Mkuu wa klabu ya KMC, Walter Harrison amesema sababu kubwa ya kuamua kucheza mchezo wao wa Ligi kuu dhidi ya Yanga Oktoba 19, 2021 mkoani Ruvuma, ni kutaka kutoa burudani ya soka kwa wakazi wa mkoa huo.

Harrison amesema ni muda mrefu sana umepita bila ya mkoa huo kushuhudia mchezo wa Ligi kuu tokea klabu ya Maji Maji ya Songea mjini ishuke daraja miaka mitatu iliyopita hivyo wakazi hao wanahamu sana ya kuona mchezo wa TPL.

"Kikubwa tulichokiona ni kuwapelekea burudani watu wa Songea kwasababu ni muda mrefu Ligi haijachezwa mkoani Ruvuma, msimu uliomalizika waliweza ku-host nusu fainali ya FA uliona mwamko ulivyokuwa”.

“Na sisi tuna nafasi ya kuwapa burudani ambayo wameimiss kwa kiasi kikubwa sana kwa muda mrefu so tunaenda pale na tukiamini kupata ushirikiano mzuri sana, tumeshakuwa kwenye mawasiliano mazuri sana ma chama cha soka cha mkoa wa Ruvuma na tutaendelea hivyo katila kufanya maandalizi na tunaamini kabisa tarehe 19 itakuwa sikukuu kubwa sana mkoani Ruvuma". Amesema Harrison.

Mara ya mwisho wawili hao kukutana ilikuwa ni kwenye michezo miwili ya ligi Kuu msimu uliopita ambapo KMC ilifungwa na Yanga 2-1 kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza  na kutoa sare ya 1-1 kwenye Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kwa michezo miwili ya Ligi iliyochezwa msimu huu, KMC ipo nafsi ya pili kutoka mwisho nafasi ya 15 ikiwa na alama 1 baada ya kucheza michezo miwili na kufunga 2-0 na Polisi Tanzania na sare dhidi ya Coastal Union.

Yanga ipo nafasi ya pili wakiwa na alama 6 sawa na kinara Polisi Tanzania baada ya Yanga kushinda michezo yake miwili dhidi ya Kagera Sukari na Geita Gold.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live