Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC vs Yanga: Aucho alitakiwa kedi nyekundu - Jemedari Said

Aucho9175 KMC vs Yanga: Aucho alitakiwa kedi nyekundu - Jemedari Said

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amesema kuwa katika mchezo wa juzi kati ya KMC dhidi ya Yanga, kiungo wa Yanga raia wa Uganda, Khalid Aucho alipaswa kupigwa kadi nyekundu mapema tu kipindi cha kwanza kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

Jemedari amesema hayo mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa ligi ambao ulipigwa katika Dimba la Jamhuri Morogoro ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 3-0.

"Unakuaje na mwamuzi wa Ligi Kuu ambaye HAJUI KUPIGANA KIWANJANI ni kosa linalostahiki RED CARD bila kujali umempiga mpinzani, mchezaji wa timu yako, mwamuzi, mshabiki, Afisa wa kiwanja, Ball kids, etc etc etc. Sasa GK wa KMC ameepukaje KADI NYEKUNDU yeye na mwenzie?

"Dakika ya 16 Khalid Aucho alimvuta kwa makusudi Awesu Awesu baada ya kupitwa, mwamuzi akapuliza filimbi ya faulo ambayo ilipaswa kuwa na kadi ya njano, lakini mwamuzi Hamisi Mdoe kutoka Tanga hakutoa hali ambayo imemsaidia Aucho kwani dakika chache baadae alifanya faulo akapewa njano, inawezekana Aucho angekuwa na Red Card kama tungekuwa na mwamuzi ambaye sio Level ya MDOE."

"Kamati ya Waamuzi na FRAT wana kazi sana na hawa waamuzi, ni hatari sana kumkuta mwamuzi KILAZA halafu anajaribu kupendelea. BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live