Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC vs Kagera Sugar hapatoshi leo

KMC Vs Kagera Sugar Leo KMC watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Kagera

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha KMC kinachodhaminiwa kinatarajia kushuka dimba la CCM Kirumba leo jumanne kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.

KMC inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa wamekusanya pointi 13 baada ya kucheza mechi tisa.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema “Mazoezi ya mwisho yamefanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa mechi na morali ya wachezaji ipo juu kuelekea kwenye mchezo huo. Tumesafiri na wachezaji 24 ambao wote wapo kwenye hali nzuri.

“Ni mchezo utakaokuwa wa ushindani kwani wapinzani wetu walipata matokeo mazuri kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania katika uwanja huu lakini hilo halituhusu kwani mchezo upo ndani ya uwezo wetu.

“Tunawaheshimu Kagera Sugar lakini mwisho wa siku tunahitaji pointi tatu kesho ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

“Tunawaomba mashabiki wa KMC mkoani Mwanza wajitokeze kuishuhudia timu yao yenye wachezaji wa VVIP.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live