Mchezo dhidi ya klabu ya Kmc na klabu ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa tarehe 22 mwezi huu ambao ilikua upigwe siku ya Jumamosi sasa rasmi utapigwa siku ya Ijumaa tarehe 21.
Taarifa hiyo imetolewa na vilabu vya KMC na Azam ambao wameeleza kua klabu hizo zitakua na mchezo huo siku hiyo ya Ijumaa badala ya jumamosi kama ratiba ya awali ilivyokua inaeleza ambapo sababu za mchezo huo kurudishwa nyumba zikielezwa.
Sababu za klabu hizo kurudisha mchezo huo nyuma ni mchezo wa tmu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 wa kufuzu michuano ya Afrika (AFCON) dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria ambao unatarajiwa kupigwa siku hiyo katika uwanja ambao ulikua utumike katika mchezo huo.
KMC ambao mchezo wao uliopita walipata matokeo mazuri dhidi ya Mtibwa Sugar ukiwa ni ushindi wao wa pili hivo jumapili wataenda kutafuta ushindi wao wa tatu mbele ya wanalambalamba Azam FC.