Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC kurudi kambini Jumamosi

Kmc+pic KMC kurudi kambini Jumamosi

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KIKOSI cha timu ya KMC kinatarajiwa kuingia kambini Jumamosi tayari kwa maandalizi ya lala salama ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21. Wanakinondoni hao walipewa mapumziko baada ya timu ya Taifa ya Tanzania kuwa na majukumu ya kitaifa sambamba na kupisha maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli anayetarajiwa kuzikwa Ijumaa. Akizungumza na Mwanaspoti Mkuu wa Idara ya Habari ya KMC Christina Mwagala amesema, kwa sasa bado wako katika maombolezo ya msiba mzito wa kitaifa na mara baada ya kupumzishwa watarejea kuendelea na maandalizi. "Kwa sasa wachezaji wetu wote wako mapumziko, ila Jumamosi watarejea kuendelea na majukumu yao kama kawaida baada ya kumpumzisha mpendwa Rais wetu Magufuli,"amesema Christina. Aidha Christina amesema, watarejea kwa kasi kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo 10 ambayo imesalia. Amesema, kwa sasa kila timu inapambana kuhakikisha inamaliza nafasi za juu ili kupata uwakilishi wa kushiriki michuano ya Kimataifa kutokana na Simba kufanya vizuri. "Tunapambana michezo hiyo 10 hata tukifanya vibaya basi iwe hata sare na sio kupoteza, maana mechi hizo ni za mwisho kumaliza msimu inatubidi tupambane vilivyo,"amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz