Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC kuishtaki Simba kwa kuwapora Awesu Awesu

Awesu Awesu Msimbazi Awesu Awesu

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya KMC umesema kuwa wameamua kuipeleka Klabu ya Simba kwenye mamla za juu za soka kwani wamewafanyia 'uhuni' kwa kumsajili mchezaji wao, kiungo fundi Awesu Awesu aliyetambulishwa na Simba SC jana.

Taarifa kutoka KMC zinaeleza kuwa, Awesu Awesu amevunja mkataba wa miaka miwili na timu hiyo, kisha kusaini Simba ambayo imepiga kambini Misri kujiandaa na msimu ujao.

Awesu alivunja mkataba wake kwa Shilingi 50 milioni, baada ya kuona ugumu wa kuondoka akiwa bado na mkataba, hivyo hakuwa na namna nyingine zaidi ya uamuzi alioufanya.

Akizungumzia hilo, CEO wa KMC FC, Daniel Mwakasungula amesema kuwa wameshangazwa na kitendo cha Simba kumtambulisha mchezaji wao kwani hawajawahi kufanya biashara yoyote na Simba SC inayomhusu Awesu.

“Huu ni uhuni ambao hauna nafasi kwenye mpira wetu kwasasa, hili sio suala la ubabe bali suala la kisheria, sisi tunapeleka suala kwenye mamlaka husika wao watakuja na mkataba wao na sisi tutakuja na mkataba wetu, tumeshangaa sana Simba kumtangaza Mchezaji wetu pasipo na kuzungumza na sisi kufanya biashara yoyote,” amesema CEO wa KMC.

Haya yanajiri huku Simba ikikabiliwa na sakata la kukiuka makubaliano wakati wa kumsajili beki wa kati wa Coastal Union, Lameck Lawi jambo ambalo mpaka sasa lipo mikononi mwa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya FFT wakati huo Lawi akiendelea kusalia Coastal.

Ndani ya msimu mmoja sajili nne za Simba zimeleta utata sijajua shida haswa ipo wapi, uelewa kwa Klabu Mama (Parent Club) kwenye mambo ya mikataba ama ni gani?

- Lameck Lawi (Coastal Union)

- Awesu Awesu (KMC)

- Valentino Mashaka (Geita)

- Yusuph Kagoma (Fountain Gate).

Sajili tatu kati ya hizo klabu zote zimelalamikiwa, inashangaza sana.

Kutua kwa Awesu ndani ya Simba kunaifanya timu hiyo kufikisha wachezaji 13 wapya waliosajiliwa kuelekea msimu ujao wa 2024-2025.

Wengine ni Joshua Mutale, Steven Mukwala, Jean Charles Ahoua, Augustine Okejepha, Deborah Fernandes, Valentino Nouma na Karaboue Chamou, Yusuph Kagoma, Omary Abdallah Omary, Valentino Mashaka, Abdulrazack Mohamed Hamza na Kelvin Kijili.

Awesu atakuwa na kazi ya ziada kufanya ndani ya kikosi cha Simba hasa eneo la kiungo mshambuliaji anapocheza kwani anakutana na ushindani wa namba kutoka kwa Edwin Balua, Ladaki Chasambi, Omary Abdallah Omary, Joshua Mutale na Jean Charles Ahoua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live