Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC chupu chupu Chamazi

KMC RUVU KMC yalazimishwa sare na Ruvu Shooting Chamazi

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la dakika ya mwisho la Charles Ilamfya limeinusuru KMC kupoteza mechi nyumbani baada ya kutoa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Ilamfya alifunga bao hilo dakika ya pili na ya mwisho ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo huo, kufuatia Ruvu Shooting kutangulia kwa bao la Ally Kombo dakika ya 22.

Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 11 katika nafasi ya 12 na Ruvu Shooting sasa ina pointi 10 katika nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 11.

Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live