Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC, Prisons hawajaonja ushindi tangu mwaka 2023 uanze

Yanga Kmc Fb KMC, Prisons hawajaonja ushindi tangu mwaka 2023 uanze

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza usiamini, ila ukweli ndio huo hadi sasa ni Tanzania Prisons na KMC pekee ambazo hazijaonja ushindi tangu mwaka 2023 uanze ikiwa ni rekodi ya kipekee kwa timu hizo katika Ligi Kuu Bara.

Prisons, miongoni mwa timu zilizofanya mabadiliko katika benchi la ufundi likianza na Mkenya, Patrick Odhiambo, sasa iko chini ya Mzanzibar Abdallah Mohamed ‘Baresi’.

Wajelajela hao wa jijini Mbeya bado hawapo nafasi nzuri wakiwa wamekusanya pointi 22 na kuwa timu tatu za mkiani sawa na Polisi Tanzania (15 ) na Ruvu Shooting inayoburuza mkia ikiwa na alama 17.

Prisons mara ya mwisho kushinda ni Desemba 25 ilipoichapa, Mbeya City 2-1 na tangu hapo ni sare na vichapo na kuiweka kwenye presha ya kushuka daraja.

Ikumbukwe timu hiyo msimu uliopita iliooangukia mchujo ‘play off’ ikapata ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania ya championship.

KMC nayo hali si salama sana wikiwa nafasi ya 12 na pointi 23 (kabla ya mechi ya jana dhidi ya Yanga) ambayo mara ya mwisho kushinda ilikuwa Desemba 22, ilipoichapa Polisi Tanzania 2-0.

Kocha wa Prisons, Baresi alisema ni muda mchache ameingia kikosini humo anafahamu ugumu lakini kubwa ni kuunganisha kwanza timu na kuwaandaa wachezaji kisaikolojia kusahau matokeo yaliyopita.

Alisema hadi sasa matokeo si mazuri na kazi ni kubwa inayohitajika ambapo nguvu si ya mtu mmoja bali umoja, ushirikiano na kujituma kwa kila mmoja kwenye nafasi yake kutimiza wajibu ili kuinusuru timu hiyo.

“Mechi zilizobaki ni vizuri tukapata ushirikiano na kila mmoja kutimiza wajibu wake, ninaamini tutabaki Ligi Kuu tukiweka malengo ya pamoja,” alisema Baresi kocha wa zamani wa Kikwajuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live