Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC, Namungo hakuna mbabe Chamazi

IMG 8982.jpeg KMC, Namungo hakuna mbabe Chamazi

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu za KMC na Namungo FC zimegawana pointi baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya KMC yamefungwa na Rahim Shomari dakika ya nne na Daruwesh Saliboko dakika ya 50, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Meddie Kagere dakika ya 57 na Ibrahim Mkoko dakika ya 61.

Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 23, ingawa inabaki nafasi ya tano na Namungo FC inafikisha pointi 20, nayo inabaki nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: