Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC Kusaka Pointi 3 zingine Leo

KMC  Thierry Hitimana Benchi la Ufundi la KMC

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya KMC inatarajia kushuka Dimbani hii leo kusaka pointi tatu zingine dhidi ya Polisi Tanzania majira ya saa 8:00 mchana katika uwanja wa Uhuru.

KMC ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo hadi sasa wakiwa wamecheza michezo 16 kwenye ligi, ushindi mara nne, sare saba na kupoteza mara tano huku wakiwa wamejikusanyia alama 19.

Wakati kwa upande wa Polisi Tanzania wao ndani ya michezo 16 waliyocheza wamejipatia pointi 9 pekee, vipigo mara 11, sare tatu na kushinda mara mbili pekee, wakiwa wanashikilia mkia.

KMC ambayo ipo chini ya Thierry Hitimana wametoka kushinda mechi yao iliyopita baada ya kukaa takribani mechi nane mfululizo bila ushindi wowote, leo hii wanakutana na Maafande ambao wana hali mbaya.

Polisi katika mechi alizobakiza akiendelea kupoteza matumaini ya kubakia ligi kuu yatakuwa hamna kutokana na ugumu wa mechi zijazo hivyo ushindi ndio kitu anachokihitaji.

Polisi ametoka kupoteza mechi nne mfululizo kwenye Ligi huku wakitafuta njia ya kufanya vizuri mechi zao zilizobakia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live