Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC FC yazitambia Simba SC, Young Africans

KMC Full Mzuka Kuwakabili Azam Kesho KMC FC yazitambia Simba SC, Young Africans

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Klabu ya KMC FC imetamba kuwa njiani kuelekea katika nafasi yake kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikiajindaa kucheza dhidi ya Mabingwa watetezi Young Africans.

KMC FC kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imejikusanyia alama 13, baada ya kuibanjua Azam FC Ijumaa (Oktoba 21), mabao 2-1 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni Christina Mwagala amesema: “Nafasi yetu karibu tunaifikia. Kuna watu mmekaa nafasi ambazo sio zenu. Sasa VVIP tunakuja hapo soon.”

Tambo hizo za KMC FC zinailenga Simba SC na Young Africans zinazolinga alama hadi sasa zikiwa nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC ipo kileleni kwa kufikisha alama 14 sawa na watani zao wa ‘JADI’ Young Africans wenye uwiyano mdogo wa mabao ya kufunga na kufungwa.

KMC FC itacheza dhidi ya Young Africans keshokutwa Jumatano (Oktoba 26) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Chanzo: Dar24