Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KMC FC yamkingia kifua David Kisu

DAVID MAPIGANO KISU KMC FC yamkingia kifua David Kisu

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Dar24

Afisa Habari wa KMC FC Christina Mwagala amewashukia Wachambuzi wa Soka la Bongo, ambao wameanzisha mjadala wa Mlinda Lango wa Klabu hiyo David Kisu Mapigano, kwa kumnyooshea kidole kufuatia kosa alilolifanya kwenye mchezo dhidi ya Young Africans jana Jumatano (Februari 22).

Mlinda Lango Kisu, alishindwa kuudaka Mpira wa Kona na kujikuta akisababisha bao la ushindi kwa Young Africans lililofungwa na Mshambuliaji Kinda Clement Mzize.

Christina Mwagala ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukiwa Wachambuzi, huku akiwataka waache tabia ya kutoa lawama kwa wachezaji, na badala yake wajenge mazoea ya kusifia mazuri pia.

Christina Mwagala ameandika: Kwa mara ya pili leo narudi tena kuzungumza na baadhi ya watu ambao wanajiita wachambuzi.

Tangu jana baada ya kumalizika kwa mchezo wetu dhidi ya Yanga ambao tulipoteza kwa goli moja kumekuwa na picha zenye maandiko ambayo sio mazuri yanatembea mitandaoni kuhusu Golikipa wetu Davidi Kisu Mapigano.

Kisu ni Golikipa mzuri na tangu tumeanza Ligi amefanya kazi kubwa sana kuisaidia Timu yetu ya @kmcfc_official na zipo mechi ngumu ambazo tumecheza na Kisu kwa nafasi yake ya Golikipa amefanya saving sana na hivyo kuisaidia Timu isipoteze baadhi ya michezo na kutoka salama.

Lakini pia kama haitoshi Kisu anashika nafasi ya pili kwakuwa na Saving nyingi akiongozwa na Hossen Abel, Mapigano ana cleenshit tano hadi sasa.

Leo hii unapokuja kuanza kumuatack mchezaji wetu kwa maneno ya interest yako unatoa wapi hiyo haki? Tunatakiwa kufahamu kwamba mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, namakosa tumeumbiwa sisi binadamu.

Mifumo Young Africans yampa jeuri NabiSasa unatoa wapi huo uthubutu wa kumsema vibaya mchezaji wetu, kwa nyie wachambuzi nani amewahi kudaka mpira mtuambie kama nyie hamjawahi kufanya makosa hadi kufikia hatua ya kumsema vibaya mchezaji wetu.

Hivi unawezaje kuandika kitu ambacho unajua kabisa kitampa shida mchezaji, Davidi kisu ukiacha kuwa ni mchezaji anafamilia , lakini pia bado ni kijana ambaye anaendelea kutafuta kupitia kipaji chake cha mpira.

Ifike wakati mtambue umuhimu wa kutumia kalamu zenu vizuri za kiuchambuzi badala ya kubomoa kwa sababu ukosoaji wenu ambao mnafanya unapelekea kumuathiri ki Synology mchezaji sio Kisu tu bali na wengine na hivyo kupoteza confidence pindi anapopata nafasi ya kucheza.

Ukosoaji wetu huo wa tuhuma unawakosesha pia wachezaji kuaminika sehemu nyingine pindi anapohitakika. Sisi hatukatai kukosolewa ila ni vizuri mnapotukosoa mtukosoe kwa heshima na staha.

Nimemaliza.

Chanzo: Dar24