Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KIBANDA UMIZA: Kiwango champonza shabiki Yanga, atimua mbio

Kibanda Umiza Pic Data KIBANDA UMIZA: Kiwango champonza shabiki Yanga, atimua mbio

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Mustafa MtupaMore by this AuthorBy Eliya SolomonMore by this Author MUDA mwingine unaweza kujiuliza kwa nini ulipenda mpira wa miguu na ukakosa jibu, yaani hutokea tu mtu unajikuta umezama kwenye mahaba haya.

Sasa shabiki mmoja wa Yanga maaufu kama Juma Yanga aliponzwa sana na kiwango cha timu yake.

Wakati mchezo wa Polisi Tanzania dhidi ya Yanga unaendelea kwenye moja ya kibanda umiza maeneo ya Buguruni Jijini Dar es salaam jamaa aliacha watu hoi kwa tukio lake la kutimua mbio.

Unaambiwa jamaa huwa Yanga ikishinda au Simba ikifungwa mashabiki wa Simba huwa hawakai kwa raha kutokana na maneno yake ya karaha.

Vile vile inasemekana aliongea maneno ya kuwaudhi sana mashabiki wa Simba baada ya kutoka sare na El Merrikh.

Hivyo, wakati mchezo unaendele yeye alikaa kwenye benchi ya nyuma kabisa na baada ya Polisi kusawazisha jamaa alitoka nduki kutoka nyuma hadi mlangoni.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz