Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KIBANDA UMIZA: Amchenjia mkewe kisa Miquissone

Kibanda 2 Pic Data KIBANDA UMIZA: Amchenjia mkewe kisa Miquissone

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KUNA watu wana vituko nyie! Shabiki mmoja wa Simba akiwa na mkewe, wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya timu yao dhidi ya Al-Merrikh, aliamua kwenda naye kutazama mchezo huo nje ya Uwanja wa Mkapa.

Shabiki huyo alitamani kuutazama mchezo huo akiwa uwanjani zuio la mashabiki kuingia uwanjani lilimfanya basi kusogea ili autazame mchezo huo akiwa karibu na uwanja huo ili walau hata baada ya mchezo awashangilie wachezaji wa timu yake.

Aliamini Simba lazima wafanye yao kwenye mchezo huo kutokana na rekodi nzuri waliyonayo kwenye michezo ya nyumbani, kama ambavyo alidhani mambo yalijipa na wekundu hao wa Msimbazi wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Wakati ambao Simba ilipata bao la kwanza lililofungwa na Luis Miquissone mke wa shabiki huyo alisimama na kusema nakupenda Mmakonde mwenzangu, ndipo jamaa alipokuja juu na kutaka kumchenjia mkewe lakini baadaye walitulizwa mashabiki hao.

Inawezekana patashika hizo zilitokea kwa sababu wakati wakitazama soka eneo hilo, walikuwa wakipata moja moto moja baridi, pengine ndio sababu ya hayo kutokea.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz