Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus wamtupia virago Kocha Massimilliano Allegri

Allegriiii Juventus wamtupia virago Kocha Massimilliano Allegri

Sat, 18 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Juventus imemfuta kazi kocha Massimiliano Allegri kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha wakati wa ushindi wa 1-0 dhidi ya Atalanta kwenye fainali ya Coppa Italia.

Licha ya kuiongoza klabu hiyo kushinda kombe hilo kwa mara ya 15 alighadhibika, kwanza akitolewa kwa kuoneshwa kadi nyekundu dakika za mwisho baada ya kuwakejeli wasimamizi wa mechi na kisha kumpuuza mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Cristiano Giuntoli wakati wa sherehe za baada ya mechi.

Paolo Montero atakuwa kocha wa muda wa klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu. Kocha wa klabu ya Bologna, Thiago Motta yupo kwenye mazungumzo na Kibibi kizee hicho cha Turin kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Allegri msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live