Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus wakubaliana na Dembélé

Ousdmane Dembele Ousmane Dembele

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Juventus imekubalina na winga wa klabu ya Barcelona Ousmane Dembélé ili kuweza kujiunga na miamba hiyo ya nchini Italia kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu.

Mkataba wa mchezaji huyo wa kifaransa unaisha mwezi June 2022 na kuanzia January atakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu yeyote, pia na kusaini mkata wa awali na klabu yeyote, mazungumzo kuhusu mkataba mpya na klabu ya Barcelona yameshindikana na leo wamefikia tamati.

Kulingana na taarifa kutoka nchini Hispania Ousmane Dembélé amekataa ofa ambayo klabu ya Barcelona wamempa kuamua kuondoka mwishoni mwa msimu kuisha.

Ousmane Dembélé japo amekubaliana na klabu ya Juventus lakini bado hajasini mkataba wowote, pia anasubili offa ya kutoka klabu ya PSG na klabu ya Manchester United na yenyewe imeshapeleka offa ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo kwa wakala wake Moussa Sissoko lakini bado haijajibiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live