Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus ugenini leo dhidi ya Verona

Ver Vs Juv Juventus ugenini leo dhidi ya Verona

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Juventus ambayo ipo chini ya Massimiliano Allegri watakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Hellas Verona ambao wapo nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Serie A baada ya kucheza michezo yao 13.

Juventus leo hii watahitaji ushindi kwa hali na mali ili waweze kutinga hadi nafasi ya 3 ya msimamo ambapo mechi yao iliyopita iliwafanya wapate hali ya kuimarika na sasa watakwenda kuzitafuta alama hizo.

Verona kati ya mechi 13 walizocheza wameshinda mechi moja, sare mbili na wamepoteza mechi 10, huku wakiwa na hati hati ya kushuka daraja endapo wataendelea na mwenendo huo.

Vijana wa Alegri wao wameshinda mechi 7, wamesare 4, na wamepoteza michezo miwili tu mpaka sasa huku wakiwa wametolewa kwenye kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na kwenda Europa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live