Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus matatani Italia, Je, watashushwa daraja

Juventus Scudetto Epa Juventus wakishangilia kuchukua kombe la Italia “Escudetto”

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la kulinda haki za mraji la Italia “CODACONS”, linadai kuwa klabu ya Juventus inaweza ikashushwa daraja kwenda kucheza Serie B na kunyang’anywa ubingwa wao wakombe la Italia kutokana na kesi inayowakabili ikiwa watatshindwa.

Juventus wanashitakiwa kwa kutoa hesabu za uongo na Marco Donzelli afichua kuwa klabu hiyo inaweza kuadhibiwa na kushushwa daraja mpaka Serie B na kufutiwa ubingwa walioshinda msimu ulioisha.

Juventus ni klabu pekee ambayo uchunguzi wake umewekwa wazi kuhusu kuongeza gharama za uhamisho, pia kuna vilabu kadhaa navyo vipo chini ya uchunguzi huo nchini Italia wa kuongeza na kudanganya thamani ya mauzo ya wachezaji vilabu hivyo ni Napoli, Roma, Atalanta, Genoa na Sampdoria.

klabu ya Biuconneri imesema itatoa ushirikiano na mamlaka zote zinazohuhusika, sababu wanaamini hawakufanya udanganyifu wowote kwenye mauzo ya wachezaji wala kununua wachezaji, sababu kulikuwa na makubaliano zaidi ya pande mbili yaliyohusu klabu na mawakala wa wachezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live