Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus kupitisha fagio Januari

Skysports Aaron Ramsey Juventus 4943754 Aron Ramsey ni miongoni mwa wachezaji wanaotaka kuuzwa Januari

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juventus wana matatizo ndani na nje ya uwanja kwa sasa, hivyo Massimiliano Allegri anatafuta suluhu.

Kocha huyo wa Kiitaliano anataka wachezaji wapya wafanye nao kazi kwenye Uwanja wa Allianz, lakini ili kupata nafasi klabu hiyo inabidi ipunguze baadhi ya kikosi chao cha sasa.

Kulingana na Corriere della Sera, Juve ina wachezaji kama wanne ambao wapo tayari kusepa Januari. Dejan Kulusevski, Aaron Ramsey, Adrien Rabiot na Arthur Melo wote wanawekwa sokoni kwa lengo la kuuzwa.

Mchezaji huyo mchanga wa Uswis amekuwa akishiriki mara kwa mara msimu huu lakini kuna imani nchini Italia kwamba Allegri hamwamini kabisa kama Andrea Pirlo.

Arthur amecheza mechi nne pekee za Serie A, na tatu kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona anasita kuondoka Bianconeri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live